28 Agosti 2012 - 06:33

Makamu wa rais wa Syria Bw Farouq al-Sharaa amesema nchi yake inatafuta utatuzi wa mgogoro nchini humo bila masharti, kwa kufuata mpango wa amani uliotolewa na aliyekuwa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa wa suala la Syria Kofi Annan.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya makamu wa rais na kuchapishwa na shirika la habari linaloiunga mkono serikali, Bw Sharaa aliwaambia maofisa kutoka Iran waliofanya ziara nchini Syria kwamba, mgogoro wa Syria unatakiwa kutatuliwa bila masharti, na pande zote zinatakiwa kuacha matumizi ya nguvu na kushiriki kwenye mazungumzo ya kitaifa.